rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uturuki Recep Tayyip Erdogan

Imechapishwa • Imehaririwa

Upinzani wataka waangalizi nusu milioni kutumwa Uturuki

media
Wafuasi wa Muharrem Ince, mgombea urais kutoka chama kikuu cha upinzani cha CHP huko Izmir, Uturuki. REUTERS/Osman Orsal

Vyama vya upinzani na mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali nchini Uturuki yana mpango wa kupeleka waangalizi zaidi ya nusu milioni kwenye vituo vya kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu siku ya Jumapili.


Wapinzani wana hofu ya kuepo udanganyifu au wizi wa kura wakati wa uchaguzi huo. Wamelaani mabadiliko ya hivi karibuni katika sheria ya uchaguzi - kadi ya uchaguzi ambayo imefanyiwa marekebisho fulani kusini-mashariki ya nchi hasa katika eneo linalokaliwa na Wakurdi - na kukumbusha madai ya udanganyifu ambayo yalizua sintofahamu katika kura ya maoni ya mwaka jana kuhusu mageuzi ya katiba.

Mpango huu unahusu kutumwa kwa waangalizi 519,000 katika vituo vya kupigia kura 180,000 nchini kote.

"Mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yamesababisha watu kutokua na imani na uchaguzi huru, wa wazi na wenye kuaminika," amesema Mbunge wa upinzani Riza Turmen, aliyekuwa jaji wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu.

"Kuachia usimamizi wa uchaguzi huu kwa kundi la watu, vikosi vya usalama na serikali badala ya vyama vya siasa kuna wasiwasi mkubwa," Riza Turmen ameongeza katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi.

Chama kikuu cha upinzani cha CHP na vyama vingine, ikiwa ni pamoja na chama chama cha Iyi, wameunda programu ya smartphone ambayo itawawezesha mawakala wao kuratibu na kutoa ripoti kwa wakati halisi kwenye zoezi la uhesabuji kura katika vituo mbalimbali vya kupigia kura siku ya Jumapili.

Mnamo mwezi Aprili 2017, Erdogan alipitisha kupitia kura ya maoni mageuzi ya Katiba yanayoimarisha madaraka yake katika nchi hiyo.