rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Indonesia Ajali

Imechapishwa • Imehaririwa

Karibu watu 200 watoweka baada ya feri kuzama Indonesia

media
Kikosi cha waokoaji wakiwaokoa waathirika baada ya feri kuzama karibu na kisiwa cha Riau Indonesia Novemba 22, 2009. REUTERS/Stringer

Abiria mia na themanini waliokua wakisafirishwa na feri ambayoilizama Jumatatu usiku wiki hii katika Ziwa Toba, Sumatra, hawajulikani walipo, mamlaka nchini Indonesia imesema leo Jumatano.


Uwezo wa feri hiyo ulikuwa mara tatu chini ya idadi hiyo na ripoti ya awali ilibaini kwamba watu 150 walitoweka. Watu kumi na nane waliokolewa mara moja baada ya feri hiyo kuzama.

"Bado tunatafuta watu 180," amesema mkurugenzi wa huduma za dharura. Utafiti huo unafanywa na kikosi cha wapiga mbizi 25.

Ziwa Toba, lenye urefu wa kilomita 100, upana wa mita 35 na mita 450 za kina, ni ziwa kubwa zaidi lenye volkano duniani. Ni sehemu muhimu ya utalii. Haijulikani kama raia wa kigeni ni miongoni mwa watu waliotoweka.