rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Korea Kaskazini China Kim Jong Un Xi Jinping

Imechapishwa • Imehaririwa

Kim Jong afanya ziara ya kushtukiza China

media
Picha ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un iliyotolewa na shirika la habari la Korea Kaskazini Kcna Juni 13, 2018 alipofika uwanja wa ndege wa Pyongyang baada ya mkutano na Rais wa Marekani Donald Trump huko Singapore. AFP

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong amefanya ziara ya kushtukiza nchini China na kupokelewa na mwenyeji wake Xi Jinping, wiki moja baada ya mkutano wa kihistoria kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini na Rais wa Marekani Donald Trump.


Televisheni ya China imerusha picha za mkutano kati ya viongozi hao wawili na wake zao katika sherehe ya mapokezi iliyofanyika katika ikulu ya rais.

Ziara hii ya kushtukizaimefanyika wakati ambapo China imekua katika mvutano mkubwa na rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mgogoro wa biashara kati ya China na Marekani, mvutano ambao umesababisha Jumanne wiki hii kushuka kwa masoko ya hisa duniani.

Hii ni ziara ya tatu ya kiongozi wa Korea Kaskazini nchini China katika kipindi kisichozidi miezi mitatu. Mwishoni mwa mwezi Machi, Bw Kim alifanya ziara yake ya kwanza nje Korea Kaskazini tangu alipochukua hatamu ya uongozi mwishoni mwa mwaka 2011, kabla ya safari ya pili mnamo mwezi Mei katikamji wa Dalian kaskazini mashariki mwa China.