rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Japani Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Tetemeko la ardhi laua watu zaidi ya watatu Osaka, Japani

media
Moja ya barabara zilizoharibiwa na tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 6.1lililopiga mji wa Osaka Jumatatu hii asubuhi, Juni 18. Twitter/@tw_hds/via REUTERS

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.1, katika vipimo vya Richter limepia mji wa Osaka, nchini Japani mapema Jumatatu asubuhi wiki hii, na kuua watu zaidi ya watatu, kulingana na ripoti ya NHK, adio na televisheni vya serikali.


Mwanamume mwenye umri wa miaka 80 na msichana mwenye umri wa miaka tisa ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba. Mtu mwengine amefariki baada ya kuangukiwa na kuta za maktaba.

Serikali imethibitisha vifo vya watu wawili.

Picha zilizorushwa na vituo vya televisheni zinaonyesha maji mengi yakifurika katika mitaa mbalimbali ya mji wa Osaka, huku nyumba moja ikiteketea kwa moto.

Tetemeko hilo lilitokea wakati raia wengii wa Japan walikua wakielekea kazini.

Waziri Mkuu Shinzo Abe amesema kuwa serikali bado inatathmini kiwango cha hasara iliyosababishwa na tetemeko hilo la ardhi na kwamba kipaumbele chake ni usalama wakaazi wa mji wa Osaka.

Hakuna onyo ya tsunami iliyotolewa. Awali Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa ilibaini kwamba ukubwa wa tetemeko la ardhi utakua wa 5.9 katika vipimo vya Richter kabla ya kubadili kauli na kusema ukumbwa wa tetemeko hilo ulikua hadi 6.1.

Tetemeko hilo limeathiri sekta muhimu ya viwanda katikati mwa Japani. Kampuni ya Panasonic, yenye makao yake makuu Osaka, imetangaza kuwa inafunga viwanda vyake viwili.

Zaidi ya familia 170,000 zimekosa umeme katika mji wa Osaka na mji jirani wa Hyogo, shirika la umeme nchini Japani limesema na kubaini kwamba umeme umerejeshwa ndani ya masaa mawili.

Daihatsu Motor, kampuni ndogo ya Toyota, imetangaza kusitisha shughuli katika viwanda vyake vya Osaka na Kyoto ili kutathimini kiwango cha hasara.

Osaka inajiandaa kupokea viongozi kutoka nchi 20 watakao shiriki mkutano wa G20 mwaka ujao.