rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Korea Kaskazini Singapore Donald Trump Kim Jong Un

Imechapishwa • Imehaririwa

Mkutano wa Singapore: Donald Trump na Kim Jong-un wasaini hati ya pamoja

media
Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakisaini hati ya pamoja katika Hoteli ya Capella katika kisiwa cha Sentosa Island, Singapore, Juni 12, 2018. REUTERS / Jonathan Ernst

Baada ya vita vya maneno na vitisho vingi vya kufuta mkutano kutoka kila upande, hatimaye mkutano wa kihistoria kati ya Marekani na Korea Kaskazini umefanyika huko Sentosa nchini Singapore Jumanne hii, Juni 12.


Mkutano huo umeanza saa tatu saa za Singapore baada ya kubadilishana maneno ya busara na kushikana mikono katika tukio la kihistoria wakati huu viongozi hawa wakimaliza awamu ya kwanza ya mazungumzo ya awali nchini Singapore. Mkutano huu wa ana kwa ana ni wa kwanza katika historia kati ya viongozi hawa nchi ambazo kwa miongo kadhaa katika uhasama.

Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili hao pekee na wakalimani wao.

Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama katika rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia.

Kwa upande wa Donald Trump, anasema hatua ya kutokomeza silaha za nyuklia itaanza "haraka sana". Rais wa Marekani anasema ameanzisha "uhusiano maalum" na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.

Wakati huo huo China imepongeza mwanzo wa 'historia mpya' kati ya Marekani na Korea Kaskazini baada ya tukio hilo la kihistoria.