rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Korea Kaskazini Marekani Kim Jong Un Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Kiongozi wa Korea Kaskazini afanya mabadiliko jeshini

media
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. KCNA via REUTERS

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amewafuta kazi maafisa watatu wa juu katika uongozi wa jeshi na kuteua wengine, kwa mujibu wa vyanzo kutoka Marekani.


Mabadiliko haya yanakuja siku chache tu kabla ya mkutano kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. Mkutano ambao umepangwa kufanyika Juni 12 huko Singapore.

Sababu za mabadiliko hayo ziko wazi, lakini kwa upande wa waangalizi wanasema hatua hii itamruhusu Kim Jong-un na chama chake, chama pekee, kuimarisha udhibiti wao katika jeshi la nchi hiyo (KPA).

"Kama Kim Jong-un anataka kushiriki mchakato wa amani na Marekani na Korea Kusini na kujadili njia ya kuondokana na mpango wa wa nyuklia, anatakiwa kupunguza ushawishi wa jeshi," amesema Ken Gause , mkurugenzi wa Kundi la Masuala ya Kimataifa katika CNA, taasisi ya utafiti na uchambuzi.

"Mabadiliko haya yamewawekakwenye mstari wa mbele maafisa ambao wana uwezo wa kufanya hivyo. Ni watiifu kwa Kim Jong-un na hakuna mtu mwingine," ameongeza.

Marekani inataka kufikia mkataba wa amani na Korea Kaskazini, na hivyo kuahidi kuifutia vikwazo vya kiuchumi na kuleta ustawi nchini Korea Kaskazini.

Maofisa wa Marekani wanaamini kwamba kuna ugomvi ndani ya jeshi kuhusu mazungumzo yaliyoanzishwa na Pyongyang,Seoul na Washington.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kusini, Yonhap, maafisa hao watatu wa juu katika uongozi wa jeshi la Korea KAskazini waliofutwa kazi ni Pak Yong-sik aliyekua akisima mia ulinzi, Ri Myong-su, mkuu wa majeshi na Kim Jong-gak, mkurugenzi wa ofisi ya kisiasa ya jeshi la Korea Kaskazini.