rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Korea Kaskazini Donald Trump Kim Jong Un

Imechapishwa • Imehaririwa

Maandalizi yaendelea kuhusu mkutano kati ya Trump na Kim

media
Mjumbe wa Korea Kaskazini Kim Yong-chol (kushoto) akikutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo (kulia) New York, Mei 31, 2018. REUTERS/Mike Segar

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kupokea barua kutoka kwa kiongozi wa Korea Kaskzini Kim Jong Un, baada ya kusema wajumbe wa Korea Kaskazini na Marekani wanaohudhuria mkutano huko jijini New York wamepiga hatua nzuri.


Barua hii itawasilishwa na afisa wa juu wa Pyongyang, Kim Yong Chol, amabaye amekuwa jijini New York katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo.

Duru zinasema katika barua hiyo, kiongozi wa Korea Kaskazini amesisitiza ahadi ya kuhakikisha kuwa nchi hiyo haiwi na silaha za nyuklia.

Trump amesema anafurihia namna mazungumzo yanavyoendelea.

Waziri Pompeo anaendelea kukutana na mjumbe wa Korea Kaskazini Kim Yong Chol.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo na afisa mwandamizi wa Korea Kaskazini Kim Yong Chol aliyekuwa afisa wa cheo cha juu wa shirika la ujasusi la Korea Kaskazini katika siku yao ya tatu ya mazungumzo wanajaribu kutafuta suluhisho la tofauti zao kati ya kuhusu mpango wa silaha za nyuklia wa Korea Kaskazini na kuleta uwezekano wa kufanyika mkutano wa kihistoria kati ya rais Donald Trump na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un.

Mikutano kati ya bwana Mike Pompeo waziri wa mambo ya nje wa Marekani na Kim Yong Chol inaendelea vizuri. Rais Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa kijeshi huko Maryland kwamba viongozi wa Korea Kaskazini wanatarajiwa leo Ijumaa kwenda mjini Washington na barua kutoka kwa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un. Ikulu ya Marekani imesema maandalizi ya mkutano wa kilele wa Juni 12 yanaendelea pamoja na kuwa rais Trump aliufutilia mbali mkutano huo mnamo tarehe 24 ya mwezi Mei. Rais Donald Trump amesema waziri wake wa mambo ya nje amekuwa na mikutano yenye tija na kwamba yeye na mjumbe huyo wa Korea Kaskazini waliendelea na mkutano mwingine siku ya Alhamisi wiki hii.