rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Korea Kaskazini Marekani

Imechapishwa • Imehaririwa

Afisa wa Korea Kaskazini yupo Marekani kuandaa mkutano wa viongozi wakuu

media
Afisa wa Juu wa Korea Kaskazini Kim Yong-chol, hapa ilikua Pyongyang, Februari 28, 2018. Patrick Semansky / POOL / AFP

Afisa wa juu katika serikali ya Korea kaskazini anafanya mazungumzo na maafisa wa Marekani ikiwa ni maandalizi ya mkutano adhimu wa nyuklia kati ya raisi Donald Trump na Kim Jong Un.


Trump alithibitisha ujio wa afisa wa korea kaskazini akisifia kuwa marekani itakuwa na jopo kabambe la majadiliano ili kumaliza hali ya sintofahamu kati ya mataifa hayo mawili.

Hata hivyo Ikulu ya white house imearifu kuwa tarehe saba mwezi ujao rais Trump atakutana na waziri mkuu wa Japan shinzo Abe kabla ya mkutano wa june 12.

Siku ya Jumatatu wiki hii afisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini alifanya ziara nchini Singapore na kukutana na maafisa wa Marekani ambapo walijadili mipango ya mkutano unaoweza kufanyika wa viongozi wakuu wa Marekani na Korea Kaskazini.

Kim Chang Son, aliyetajwa na chombo cha habari cha Korea Kusini kama "mtumishi mkuu" wa kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un aliwasili katika mji wa Singapore kupitia Beijing siku ya Jumatatu.