Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

China: Tuko tayari kuleta amani katika rasi ya Korea

"Kufutwa kwa mkutano wa kilele kati ya Kim Jong-in na Donald Trump ni pigo kubwa kwa maendeleo katika rasi ya Korea," vyombo vya habari vya China vimeeleza Ijuma hii Mei 25. Kwa sasa, China bado haijasema chochote, lakini maneno yake ya mara kwa mara "China iko tayari kwa kuleta amani katika rasi ya Korea" yameendelea kugonga vichwa vya habari nchini humo.

Rais wa China na Xi Jinping na mwezake wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Machi 28, Beijing.
Rais wa China na Xi Jinping na mwezake wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Machi 28, Beijing. CCTV / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump alimwandikia barua Kiongozi wa Korea Kaskazini barua na kumwambia kuwa, mkutano wa ana kwa ana uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 12 mwezi ujao, hautafanyika tena.

Trump alisema amefikia uamuzi huo kwa sababu ya majibu ya hasira kutoka Pyongyang hivi karibuni, na hivyo isingekuwa vema kuendelea na mkutano huo.

Hatua hii ya Marekani inaweza kuwagawa washirika wa Marekani katika mchakato wa amani katika rasi ya Korea, hasa nchi kutoka bara la Asia zilizo irani ya Kora Kaskazini.

Hatua ya rais wa Marekani imewagusa wengi hasa, China, Korea Kusini na jumuiya ya kitaifa, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja w Mataifa Antonio Guterres, ameelezea kuguswa kwake na hatua hiyo ya Marekani huku naye rais wa Korea Kusini Moon Jae-In akitoa wito wa kuwepo kwa mkutano wa dharura wa viongozi wa juu wa usalama kuhusiana na suala hilo.

Marekani inailaumu Korea Kaskazini kwamba haikuwa imara katika maandalizi na kwamba pale maofisa wa Marekani walipopanga kukutana na wanadiplomasia wa Korea kaskazini hawakutokea, dalili zilizokuwa mbaya kuelekea mazungumzo haya.

Hata hivyo yapo baadhi ya mambo yanayotajwa kama dosari zilizo jionyesha kuelekea mazungumzo hayo na hasa kauli za kushinikiza msimamo wake ndani ya barua aliyomuandikia kiongozi wa Korea Kaskazini baada ya kuwa na mazungumzo na rais wa Korea Kusini Moon.

Mkutano huu ungejadili namna ya uondoaji wa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea kufuatia mkutano wa Korea zote mbili uliofanyika mwezi April mwaka huu.

Uamuzi huu ulikuja, katika siku ambayo Korea Kaskazini imeharibu kituo cha kujaribia silaha zake za nyuklia katika eneo la Pungeri mbele ya wanahabari wa Kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.