Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-USALAMA

Pyongyang yaanza zoezi la kuharibu kituo cha majaribio ya nyuklia cha Punggye-ri

Korea Kaskazini imeanza Alhamisi wiki hii zoezi la kuharibu kituo chake kikuuu cha silaha za nyuklia cha Punggye-ri, vyombo vya habari vya Korea Kusini vimebaini.

Serikali ya Korea Kaskazini imealika waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali thelathini tano: Marekani, China, Urusi, Korea Kusini na Uingereza kuhudhuria zoezi la kuharibu kituo kikuu cha majaribio ya silaha za nyuklia cha Punggye-ri.
Serikali ya Korea Kaskazini imealika waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali thelathini tano: Marekani, China, Urusi, Korea Kusini na Uingereza kuhudhuria zoezi la kuharibu kituo kikuu cha majaribio ya silaha za nyuklia cha Punggye-ri. /REUTERS/DigitalGlobe
Matangazo ya kibiashara

silaha za nyuklia, kama sehemu ya jitihada zake za kutoendelea kutengwa kimataifa, wakati ambapo kiongozi wa Korea Kaskazini Kaskazini Kim Jong-un anatarajiwa kukutana na Donald Trump kwa mkutano wa kihistoria mnamo Juni 12 katika mji wa Singapore.

Tangu mwaka 2006, Pyongyang imefanya majaribio yake sita ya nyuklia kwenye kituo hiki, ambacho ni mfululizo wa maeneo yaliyochimwa ardhini chini ya Mlima wa Mantap kaskazini mashariki mwa Korea Kaskazini.

Serikali ya Korea Kaskazini imealika waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali thelathini tano: Marekani, China, Urusi, Korea Kusini na Uingereza.

Wamekuja kuhudhuria milipuko hiyo ya kuharibu vituo hivyo vya majaribio, Kaskazini-Mashariki mwa nchi, kwenye kituo hicho kikuu, kwenye mlima, ambapo serikali ilitekeleza milipuko sita ya kinyuklia tangu mwaka 2006 hadi mwaka jana.

Lakini waandishi hawa wa habari wa kigeni wako chini ya uangalizi mkali na hawana uwezo wowote wa kuendesha kazi halisi ya uchunguzi.

Baada ya kuwasili kwao katika Uwanja wa Ndege wa Wonsan, simu zao na vifaa vyao mbalimbali vimechukuliwa na mamlaka husika, amesema mwandishi kutoka kituo cha Sky News kutoka Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.