rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

Korea Kaskazini Kim Jong Un

Imechapishwa • Imehaririwa

Korea Kaskazini yaanza kuharibu silaha zake za nyuklia

media
Waandishi wa habari wa Korea Kusini wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Wonsan wakitokea Seoul, Mei 23, 2018. News1 via REUTERS

Katika rasi ya Korea, maandalizi yanaendelea kwa ajili ya kuharibu kituo kikuu cha majaribio ya silaha za nyuklia cha Korea Kaskazini. Serikali ya Kim Jong-un imealika vyombo vya habari kumi vya kigeni kuhudhuria moja kwa moja zoezi hilo la kuharibu vituo vilivyotumika katika milipuko sita ya nyuklia ya ardhini tangu mwaka 2006.


Serikali ya Korea Kaskazini imealika waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali thelathini tano: Marekani, China, Urusi, Korea Kusini na Uingereza.

Wamekuja kuhudhuria milipuko hiyo ya kuharibu vituo hivyo vya majaribio, Kaskazini-Mashariki mwa nchi, kwenye kituo hicho kikuu, kwenye mlima, ambapo serikali ilitekeleza milipuko sita ya kinyuklia tangu mwaka 2006 hadi mwaka jana.

Lakini waandishi hawa wa habari wa kigeni wako chini ya uangalizi mkali na hawana uwezo wowote wa kuendesha kazi halisi ya uchunguzi.

Baada ya kuwasili kwao katika Uwanja wa Ndege wa Wonsan, simu zao na vifaa vyao mbalimbali vimechukuliwa na mamlaka husika, amesema mwandishi kutoka kituo cha Sky News kutoka Uingereza.