Pata taarifa kuu
THAILAND-USALAMA-SIASA

Upinzani waandamana Bangkok miaka minne baada ya jaribio la mapinduzi

Makabiliano yametokea kati ya vikosi vya usalama vya Thailand na waandamanaji wanaodai kufanyika kwa uchaguzi mnamo mwezi Novemba mwaka huu. Makabiliano hayo yametokea wakati wa maandamano ya maadhimisho ya miaka minne ya mapinduzi ya jeshi Mei 22, 2014.

Polisi ya Thailand ikikabiliana na waandamanaji Bangkok, Mei 22, 2014.
Polisi ya Thailand ikikabiliana na waandamanaji Bangkok, Mei 22, 2014. REUTERS/Athit Perawongmetha
Matangazo ya kibiashara

Awali Utawala wa kijeshi ulionya waandamanaji na mkusanyiko wowote wa hadhara uliopigwa marufuku nchini humo.

Polisi imesema, maandamano yaliyoanzia Chuo Kikuu cha Thammasat, yalijumuisha watu 500.

Waandamanaji walitarajia kwenda hadi makao makuu ya serikali lakini eneo hilohilo lilikuwa limezingirwa kabla na polisi.

Waandamanaji wachache walijaribu kuvuka kwa nguvu eneo hilo kabla ya kuachana na mpango huo. Wengi wao walipoteza fahamu na baadhi walisafirishwa na magari ya wagonjwa hadi hospitali, waandishi wa habari nchini humo wamearifu.

Utawala huo wa kijeshi unaojulikana kama Baraza la Kitaifa la Amani na Usalama (NCPC), ulitangaza katika taarifa yake kuwa umeanzisha mchakato wa kuwafungulia mashitaka watu watano wanaoshutumiwa kuandaa maandamano hayo.

Utawala wa kijeshi nchini Thailand umeahirisha mara kadhaa tarehe ya uchaguzi mkuu, na sasa umeahidi kuwa uchaguzi huo utafanyika manamo mwezi Februari 2019 baada ya kutangazwa kufanyika mnamo mwezi Novemba 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.