rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Urusi Ujerumani Vladimir Putin Angela Merkel

Imechapishwa • Imehaririwa

Vladimir Putin kukutana na Angela Merkel

media
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Sochi, Mei 2, 2017. REUTERS/Alexander Zemlianichenko

Rais wa Urusi Vladimir Putin na Angela Merkel watatarajia kukutana Ijumaa wiki hii mjini Sochi, kwenye mwambao wa Bahari Nyeusi. Masuala kadhaa yatajadiliwa: Ukraine, Syria, lakini pia mpango wa nyuklia wa Iran.


Vladimir Putin na Angela Merkel wanafahamiana vizuri, wamekutana kwa zaidi ya miaka kumi na miwili katika mikutano ya kimataifa.

Masuala yanayozua tofauti kati ya viongozi hawa wawili ni mengi. Waili hawa waliwahi hata kushambuliana katika miaka kadhaa iliyopita, kuhusu masuala ya Syria na Ukraine, mmoja akitaka kuchukuliwa vikwazo vya Ulaya na mwengine akitaka vikwazo visichukuliwe.

Lakini uamuzi wa Donald Trump wa kujitoa kwenye mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran unaweza kujadiliwa katika mkutano huo. Ujerumani, kama nchi zote za Ulaya, zilishtumu uamuzi huo. Vladimir Putin pia anatarajia kufanya kilio chini ya uwezo wake ili kuokoa mkataba huo, jambo hilo linaweza kuwa na makubaliano makubwa kati ya kiongozi wa Ujerumani na rais wa Urusi.

Mkutano huu wa kwanza na kiongozi wa Ulaya, wiki moja kabla ya Emmanuel Macron kuzuru nchini Urusi, itakuwa fursa kwa Rais wa Urusi kupima madhara ya kidiplomasia kkwa nchi za Ulaya na Marekani.