rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Armenia Nikol Pachini

Imechapishwa • Imehaririwa

Kiongozi wa upinzani achaguliwa kuwa Waziri Mkuu Armenia

media
Nikol Pachini, Waziri Mkuu mpya akisalimu umati wa wafuasi wake kwenye eneo la Jamhuri huko Yerevan, Mei 8, 2018. Sergei GAPON / AFP

Nchini Armenia, bunge limemchagua kiongozi wa upinzani Nikol Pachini kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, wakati ambapo Armenia imekua ikiendelea kukumbwa kwa wiki tatu na maandamano ya kuipinga serikali.


Nikol Pachini alikuwa mgombea pekee katika mbio ya kinyang'anyiro cha nafasi hii. Uchaguzi wake umekaribishwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Katika mji wa Yerevan, wafuasi wa Nikol Pachini walikusanyika kwenye eneo la Jamhuri ya Jumapili asubuhi Jumanne wiki hii wakisubiri uchaguzi huo ambao ulikua ukirushwa moja kwa moja kwenye redio na televisheni.

"Tunafurahi kwa sababu tunataka nchi hii kuwa na maandeleo, pia tulitaka uhuru zaidi" na hivi ndivyo Waziri Mkuu mpya alivyoahidi wakati wa kampeni yake, raia mmoja wa Armenia mwenye asili ya Ufaransa amesema.

Shahidi mmoja ambaye amekaribisha njia iliyotumiwa na Bw. Pachini, ambaye "tangu mwanzo wa harakati zake, aliomba waandamanaji kuheshimu taasisi, na kuepukana na vurugu. Jambo hilo ni zuri na watu walifuata kwa makini maneno yake. "

"Nina furaha sana kwa nchi yangu. Tulisubiri hili kwa muda mrefu sana, "alisema mmoja wa waandamanaji aliyekua alivalia nguo nyeupe. Rangi ambayo iliyochaguliwa kama ishara ya matumaini na waandamanaji ambao wataendelea kusherehekeaushindi huo hadi Jumatano wiki hii.

Nikol Pachini alichaguliwa kwenye nafasi ya waziri mkuu kwa kura 59 katika bunge

Mbunge wa upinzani na mwandishi wa zamani mwenye umri wa miaka 42 alionekana mbele ya wenzao kwa mara ya pili katika siku nane za mandamano, baada ya kushindwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita. Nikol Pachini alipata kura 59 dhidi ya 42. Alihitaji uungwaji mkono wa wabunge 53. Wabunge wa Chama cha Republican walimpa kura 11 ili kuruhusu uchaguzi wake baada ya kukataa kumpigia kura mnamo Mei 1.

Kwa upane wa wabunge hao wanasema walitaka kuepuka bunge lisivunjwi ikiwa hakutofikiwa makubaliano kuhusu jina la Waziri Mkuu. "Bado tunapinga Nikol Pachini kwenye nafasi ya waziri mkuu, lakini muhimu zaidi kwetu ni kuhakikisha utulivu nchini," kiongozi wa kundi la wabunge wa chama cha Republican Vagram Bagdassarian, ameliambia shirik la habari la AFP muda mfupi kabla ya kura hiyo kupigwa.

Nikol Pachini, aliyechaguliwa kuwa Waziri Mkuu mpya Jumanne Mei 8, akipongezwa na wabunge kutoka chama chake katika Bunge la Armenia. KAREN MINASYAN/AFP