rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Japani Korea Kaskazini Moon Jae-in

Imechapishwa • Imehaririwa

Japani na Korea Kaskazini zaanza tena mazungumzo

media
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in (kulia) na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wako tayari kuleta amani katika rasi ya Korea. Korea Summit Press Pool/Pool via Reuters

Japani na Korea ya Kaskazini zinatarajiwa kuanza tena mazungumzo na kuimarisha uhusiano ili kuchangia kwa kuleta amani na utulivu katika ukanda huo, Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ameliambia gazeti la Japani la Yomiuri Jumanne wiki hii.


"Ikiwa uhusiano kati ya Japani na Korea Kaskazini ulikuwa sio wa kawaida, unaweza kuchangia sana katika kuleta amani na usalama katika Asia ya Kaskazini, mbali na rasi ya Korea," Moon Jae-in amesema, akiandika maswali yaliyowasilishwa na gazeti la Yomiuri.

Siku ya Jumapili, Jae-in atahudhuria mkutano wa kilele huko Tokyo pamoja na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe na Waziri wa China Li Keqiang. Swali la Korea Kaskazini litawekwa kwenye ajenda ya mazungumzo.

Katika mkutano wa kwanza kati ya Korea mbili kuhusu rasi ya Korea kwa zaidi ya muongo mmoja mwezi uliopita, viongozi wa nchi hizi mbili waliahidi kuchangia katika kuleta amani na usalama katika rasi ya Korea.

Rais wa Korea Kusini pia atakutana na Rais wa Marekani Donald Trump.