rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Urusi Vladimir Putin Dmitry Medvedev

Imechapishwa • Imehaririwa

Vladimir Putin apendekeza Dmitry Medvedev kuwa Waziri Mkuu

media
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu Dmitry Medvedev wakati wa mkutano wao huko Crimea, Agosti 19, 2016. REUTERS/Dmitry Astakhov

Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye ameapishwa Jumatatu asubuhi wiki hii kama rais wa Urusi kwa muhula wa nne, amependekeza Dmitry Medvedev kuendelea kushikilia nafasi yake ya waziri mkuu, Kremlin imetangaza kwenye tovuti yake.


Dmitry Medvedev mwenye umri wa miaka 52, ambaye amekuwa amekua akihudumu kama waziri mkuu tangu mwaka 2012, alijiuzulu masaa machache mapema leo Jumatatu, pamoja na mawaziri wengine wa serikali, kwa mujibu wa utaratibu.

Jina la Dmitry Medvedev linatarajiwa kupitishwa na bunge (Duma).

Bw Medvedev alizaliwa huko St. Petersburg - wakati huo ikiitwa Leningrad - kama Vladimir Putin, na alifanya kazi naye katika manispaa ya mji mkuu wa pili wa Urusi katika miaka ya 1990.

Dmitry Medvedev baada ya kuwa mshirika wa karibu wa Rais Putin katika miaka ya 2000, aliweza kuchukua nafasi yake ya urais mwaka 2008, kwa sababu wakati huo sheria haikumruhusu kuwania zaidi ya mihula miwil mfululizo. Tangu mwaka 2012, Vladimir Putin alirudi kuchukua nafasi ya urais, huku Dmitry Medvedev akiteuliwa kama Waziri Mkuu.