rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Urusi Vladimir Putin

Imechapishwa • Imehaririwa

Rais wa Urusi aapishwa kwa muhula wa nne

media
Rais wa Urusi Vladimir Putin, Aprili 11, 2018. Sergei Ilnitsky/Pool via REUTERS

Rais wa Vladimir Putin ameapishwa kwa muhula wa nne kama rais wa nchi hiyo. Sherehe hiyo ya kuapishwa kwake imefanyika Jumatatu wiki hii katika ukulu ya Kremlin mjini Moscow na watu wa karibu yake tu ndio waliohudhuria sherehe hiyo ikilinganishwa na ile ya mwaka 2012, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.


Kumekuwa na hofu kwamba huenda kutazuka ghasia tena leo Jumatau wakati anapoapishwa.

Siku ya Jumamosi polisi wa kupambana na fujo walikabiliana na waandamanaji wanaopinga utawala wake mjini Moscow na katika miji mingine.

Vladimir Putin amekuwa madarakani kwa miaka 18 sasa kama rais wa nchi hiyo na aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu. Hata hivyo wapinzani wamekua wakikosoa utawala wake na kufananisha muda wake wa uongozi kama utawala wa mfalme.

"Nitafanya kilio chini ya uwezo wangu ili kuongeza nguvu, ustawi na utukufu wa Urusi", amesema Bw. Poutine, mbele ya wabunge, wanaseneta na viongozi nyanja za utamaduni za Urusi waliokusanyika katika ikulu ya Kremlin.

Aliwashukuru Warusi waliomuunga "mkono", akibaini kwamba hali hii ni "muhimu sio tu kwa ajili ya ulinzi wa msimamo wetu kwenye nyanja ya kimataifa, lakini pia kwa mabadiliko chanya yenye kina ndani ya nchi".

"Kama kiongozi anatetea maslahi ya nchi yake, anafaa kubaki madarakani milele hadi kifo chake," Maxime Kouznetsov, mmoja wa washirika wa karibu wa putin , ameliambia shirika la habari la AFP.

Rais wa kwanza aliyechaguliwa mnamo mwaka 2000, Putin aliwania tena muhula mwingine mnamo mwaka 2004 kabla ya kujiuzulu 2008 ili kuhudumu kama waziri mkuu chini ya mshirika wake Dmitry Medvedev, kwa sababu kisheria, alikua anaruhusiwa kuhudumu kwa mihula miwili pekee.

Iwapo atakapofika mwisho wa muhula wake wa nne mwaka 2024, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 atakuwa amehudumu kwa takriban robo karne.