Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-NYUKLIA-USALAMA

Iran yaonya kutotekeleza mkataba wa kusitisha mradi wake wa nyuklia

Balozi wa Iran nchini Uingereza Hamid Bae-dine-jad, ameonya kuwa nchi yake itaacha kutekeleza mkataba wa kusitisha mradi wake wa nyuklia iwapo Marekani itaamua kujiondoa kwenye mkataba huo.

Vienna, picha ya viongozi wa nchi zilizopelekea mkataba wa kihistoria wa kuizuia Tehran kusitisha mradi wake kwa muda wa miaka 10 ili kupunguza uwezekano wa taifa hilo kutengeneza silaha za maangamizi.
Vienna, picha ya viongozi wa nchi zilizopelekea mkataba wa kihistoria wa kuizuia Tehran kusitisha mradi wake kwa muda wa miaka 10 ili kupunguza uwezekano wa taifa hilo kutengeneza silaha za maangamizi. REUTERS/Joe Klamar/Pool
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akikosoa mkataba huo na kuna hofu kuwa huenda akaamua kuiondoa nchi yake kwenye mkataba huo tarehe 12 mwezi huu.

Mkataba huo ulitiwa saini kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani, kwa lengo la kuizuia Tehran kusitisha mradi wake kwa muda wa miaka 10 ili kupunguza uwezekano wa taifa hilo kutengeneza silaha za maangamizi.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitaka Marekani kutojiondoa kutoka katika mkataba wa kimataifa uliopangwa kudhibiti uwezo wa nyuklia ya Iran.

Guterres amesema makubaliano ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu hayapaswi kutelekezwa isipokuwa kuwe na mbadala mwingine mzuri zaidi.

Viongozi wa Ulaya wamemtaka pia Rais Donald Trump wa Marekani kubakia katika makubaliano hayo.

Rais huyo wa Marekani aliyaita makubaliano hayo kwamba ni mkataba mbaya zaidi na kuonesha nia ya kutaka kujitoa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.