rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Korea Kaskazini Korea Kusini Kim Jong Un Moon Jae-in

Imechapishwa • Imehaririwa

Kim na Moon wafanya mazungumzo ya kihistoria

media
Kim Jong-un na Moon Jae-in wakipeana mkono, Panmunjom tarehe 27 Aprili, 2018. Host Broadcaster via REUTERS TV

Viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini, wameshakutana na wanazungumzia ajenda ambazo walikubaliana awali kabla ya mkutano lakini baadae watazungumza kuhusu masuala ya kibishara kama ilivyo kwenye ajenda.

 

 


Mkutano huu umeanza kwa lengo la kupata amani kati ya mataifa hayo mawili yaliyokua katika uhasama kwa miongo kadhaa.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae, wameonekana wakisaliamina wakiwa na tabasamu kubwa.

Kiongozi wa Korea Kusini amesema ana furaha kubwa kukutana na mwenzake na wana nia ya dhati ya kupata mwafaka na kumaliza vita ambavyo vimekuwa vikiendelea nchini humo tangu mwaka 1953.

Ajenda kuu ya mkutano huu wa kihistoria ni kujadili mradi wa nyuklia wa Korea Kaskazini ambao umekuwa ukitishia usalama wa Korea Kusini kwa lengo la kupata amani ya kudumu.

Marekani imesema imefurahishwa na mkutano huu ambao, Washington DC wanasema utakuja na mkataba wa amani.

Matumaini ya pande hizi mbili kuja pamoja, yalianza kuonekana baada ya Korea Kusini kuruhusu Korea Kaskazini kutuma wanamichezo wake kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi mapema mwaka huu.