rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Bosnia Herzegovina

Imechapishwa • Imehaririwa

Kesi ya rufaa ya Radovan Karadzic kufunguliwa Jumatatu hii

media
Kiongozi wa zamani wa Waserbia wa Bosnia, Radovan Karadzic. REUTERS/Michael Kooren

Kiongozi wa zamani wa Waserbia huko Bosnia, Radovan Karadzic, atafikishwa Jumatatu wiki hii mbele ya mahakama ya kimataifa miaka miwili baada ya kuhukumiwa miaka 40 jela kwa mauaji ya kimbari, ikiwa ni pamoja na kuhusika kwake katika mauaji ya Srebrenica mnamo mwaka 1995.


Kiongozi huyo wa zamani, mwenye umri wa miaka 72, mtawala mkuu ambaye hajawahi kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa kwa Yougoslavia (ICTY), amekata rufaa dhidi ya hukumu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea mnamo mwezi Julai 1995 huko Srebrenica, "eneo la usalama" lililokua chini ya ulinzi wa Umoja wa Mataifa, ambapo Waislam 8,000 wa Bosnia, watu wazima na vijana, waliuawa na kundi Waserbia wa Bosnia.

Pia alpatikana na hatia ya makosa mengine tisa ya uhalifu wa kivita.

Radovan Karadzic amefanya orodha ya malalamiko hamsini ambapo anasem anataka yaweze kufuta hukumu hiyo dhidi yake.

Kama katika mahakama ya kwanza, Radovan Karadzic ameamua kusimama peke yake kwa kujitetea.