rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Korea Kusini Park Geun-Hye

Imechapishwa • Imehaririwa

Rais wa zamani wa Korea Kusini ahukumiwa kifungo cha miaka 24

media
Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun-hye akishikiliwa na vyombo husika kwa kosa la rushwa. REUTERS/Kim Hong-Ji

Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun-hye amehukumiwa na Mahakama ya Seoul kifungo cha miaka 24 baada ya kutwa na hatia ya rushwa kwa kuhusika kwake katika kashfa kubwa ya ushawishi wa bishara ambao ulisababisha mdororo wa uchumi wa nchi hiyo.


Mahakama imeamua leo Ijumaa kuwa kiongozi huyo wa zamani alikubaliana na rafiki yake Choi Soon-sil kupokea fedha kutoka kwa makampuni ya Korea Kusini, ikiwa ni pamoja na Samsung na Lotte.

Park, mwenye umri wa miaka miaka 66, ambaye alitimuliwa madarakani mnamo mwezi Machi 2017, alishtakiwa kwa kosa la rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na vitisho. Park ambaye hakuepo wakati wa uamuzi wa mahakama, amekanusha shtuma hizo dhidi yake.

awali Ofisi ya mwendesha mashitaka iliomba Park Geun-hye kufungwa miaka 30 na kulipa faini ya Wons bilioni 118.5, sawa na Dola milioni 127.

Rafiki na msiri wake Choi Soon-sil, anayehusika katika kashfa hiyo, alihukumiwa mnamo mwezi Februari kufungwa jela miaka 20.