Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-CHINA

Uvumi wazidi kuenea kuwa Kim Jong-Un kafanya ziara ya siri China

Taariza za uvumi kuhusu kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un kuwa yuko ziarani nchini China zimeendelea kuenea kwa kasi baada ya chombo kimoja cha habari nchini Japan kuripoti kuwa treni moja maalumu ya Korea Kaskazini ilipokelewa kwa heshima zote za kijeshi chini ya ulinzi mkali.

Kiongozi wa Korea Kasakzini Kim Jong Un wakati alipokutana na ujumbe wa Korea Kusini, Machi 6, 2018.
Kiongozi wa Korea Kasakzini Kim Jong Un wakati alipokutana na ujumbe wa Korea Kusini, Machi 6, 2018. KCNA/via Reuters/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa taarifa hizi zitathibitishwa itakuwa ni ziara ya kwanza ya Kim Jong-Un nje ya nchi yake tangu aingie madarakani mwaka 2011 na itabadili kabisa uelekea wa kidiplomasia kwenye eneo hilo tangu kufanyika kwa michezo ya Olimpiki nchini Korea Kusini.

Taarifa hizi zinaenea wakati huu Korea Kaskazini ikiripotiwa kuwa tayari kuwa na mazungumzo na nchi ya Marekani pamoja na jirani yake Korea Kusini kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo wamekuwa wakidai kuwa nchi ya China ambayo ni mshirika mkubwa na rafiki wa karibu wa Korea Kaskazini imetengwa katika juhudi za hivi karibuni na ziara ya Kim itairejesha China katika ramani ya mazungumzo haya.

Uwezekano wa ziara hii uliripotiwa kwa mara ya kwanza na shirika la habari la Japan Kyodo ikinukuu mtoa taarifa mmoja aliyedai hivi karibuni ujumbe wa juu wa Korea Kaskazini utatembelea China.

Kituo cha televisheni cha Japan Nippon kimeonesha picha za video za treni iliyotumiwa na baba wa Kim, Kim Jong Il wakati alipofanya ziara mjini Beijing na kupokelewa kwa gwaride la heshima.

Meneja wa duka moja lililoko kwenye kituo hicho cha Treni amesema walizuiwa kwa muda wote wa mchana huku kukiwa na ulinzi mkali wa polisi.

Katika nyumba ya kulala wageni ya Diaoyutai ambayo Kim Jong Il alilala wakati wa ziara yake Biejing, kulikuwa na ulinzi usio wa kawaida ambapo polisi walikuwa wametawanywa kila mita 50 hadi 100 kutoka kwenye nyumba hiyo.

Mwandishi wa habari wa AFP ameripoti kuwa aliona msafara wa magari kama yanayotumiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini ukiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.