Pata taarifa kuu
MYANMAR

Rais wa Myanmar Htin Kyaw ajizulu, kiongozi mpya kuchaguliwa ndani ya siku 7

Rais wa Myanmar Htin Kyaw ametangaza uamuzi wa kushtukiza kwa kujiuzulu nafasi yake Jumatano ya wiki hii, akimuacha kiongozi wake Aung San Suu Kyi bila ya kuwa na mshirika wa karibu kisiasa wakati huu akikabiliwa na shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa kuhusu machafuko ya kwenye jimbo la Rakhine.

Rais wa Myanmar, Htin Kyaw. Desemba 14, 2017
Rais wa Myanmar, Htin Kyaw. Desemba 14, 2017 © REUTERS/Franck Robichon/Pool
Matangazo ya kibiashara

Rais Kyaw ambaye ni rafiki wa muda mrefu wa Suu Kyi, alichukua hatamu ya uongozi baada ya yeye kukataliwa kuongoza taifa hilo kwa mujibu wa katiba iliyoandaliwa na jeshi.

Nafasi yake haikuwa na nguvu sana huku Suu Kyi ndie akiwa mtendaji mkuu wa Serikali anayefanya maamuzi katika utawala wa kiraia.

Hata hivyo Kyaw mbali na kutokuwa na mamlaka ya juu lakini alikuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za ndani ya nchi hiyo na mtu wa karibu wa Suu Kyi na chama chao.

Makamu wa rais wa Myanmar Myint Swe, jenerali mstaafu wa jeshi wakati wa utawala wa Than Shwe, atakaimu nafasi hiyo kwa muda hadi pale rais mpya atakapochaguliwa kwa mujibu wa katiba.

Kwa miezi kadhaa sasa kulikuwa na uvumi kuhusu kuzorota kwa afya ya Kyaw mwenye umri wa miaka 72 ambaye hivi karibuni alipoteza uzito na kupata matatizo ya moyo.

Taarifa iliyocahposhwa kwenye mtandao rasmi wa Serikali wa facebook, imesema rais U Htin Kyaw amejizulu nafasi yake machi 21.

Taarifa hiyo ikaongeza kuwa rais mpya atachaguliwa kaika kipindi cha siku 7 zijazo.

Punde baada ya kujiuzulu kwa rais Kyaw, spika wa bunge la wawakilishi na mshirika wa karibu wa Suu Kyi nae akatangaza kujiuzulu akitoa nafasi ya kuchaguliwa kuwa mrithi wa nafasi ya urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.