Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI

Wanamuziki wa Korea Kusini kufanya onesho la kwanza Korea Kaskazini

Wanamuziki maarufu wa Korea Kusini, K-Pop wanatarajiwa kufanya onyesho lao la kwanza nchini Korea Kaskazini ikiwa ni zaidi ya muongo mmoja, wamesema maofisa wa Serikali wakati huu uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukiwa umebadilika tangu makubaliano ya kuelekea michezo ya Olimpiki iliyomalizika mwezi mmoja uliopita.

Kundi la wanamuziki maarufu wanawake wa Korea Kusini, K-pop. Hapa ilikuwa ni mwaka 2012
Kundi la wanamuziki maarufu wanawake wa Korea Kusini, K-pop. Hapa ilikuwa ni mwaka 2012 Canal +
Matangazo ya kibiashara

Seoul itatuma zaidi ya wanamuziki 160 kwenda Pyongyang kwa ziara ya siku nne kuanzia Machi 31 hadi April 3, imesema taarifa iliyotolewa na kamati ya ushirikiano wa nchi hizo mbili kwenye eneo la kijiji cha Panmunjom.

Kundi hilo litajumuisha mwanamuziki mkongwe Cho Yong-pil na Choi Jin-Hee, wanamuziki watano wa kundi la muziki wa Pop, K-Pop pamoja na Seohyun mwanamuziki wa muda mrefu katika kundi la wanamuziki wanawake la k-Pop.

Wanamuziki hawa watafanya onyesho lao la kwanza kwenye ardhi ya Korea Kaskazini tangu mwaka 2007.

“Haikuwa rahisi kuchagua nyimbo ambazo zilitakiwa na pande zote mbili,” amesema Yoon Sanga mkuu wa ujumbe wa mazungumzo kati ya nchi hizo mbili.

Seoul imesema kuwa utawala wa Pyongyang uliwaalika wanamuziki hao kwa lengo la kuendeleza mshikamano na mchakato wa amani ulioanzia wakati wa michezo ya Olimpiki na baadae ujumbe wa Korea Kusini kukutana na Kim Jong-Un.

Utawala wa Korea Kaskazini ulituma timu ya wanamuziki wake kwenda Korea Kusini wakati wa michezo ya Olimpiki ambapo jumla ya wanamuziki wa bendi maarufu 140 walionesha ufundi wao.

Bendi ya Korea Kusini itafanya maonesho mawili kwenye ukumbi wenye uwezo wa kubeba mashabiki 1500 mashariki mwa mji wa Pyongyang na kwenye mji wa Ryugyong Jong Ju Yong ambao unaweza kuhimili mashabiki elfu 12.

Maonesho haya yamekuja ikiwa zimebaki siku chache tu kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi kutoka pande hizo mbili mapema mwezi April kwenye eneo la Panmunjom.

Mwaka 1085 wanamuziki wa Korea Kusini walifanya onesho lao la kwanza mjini Pyongyang kama sehemu ya kubadilishana tamaduni.

Kutokana na mkutano wa kihistoria kati ya utawala wa Seoul na Pyongyang mwaka 2000, baadhi ya waimbaji wa Korea akiwemo Cho Yong-pil walifanya onesho Korea Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.