Pata taarifa kuu
UFILIPINO-ICC-DUTERTE

Rais Duterte kuiondoa Ufilipino katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema nchi yake itajiondoa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Jengo la mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC.
Jengo la mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC. REUTERS/Jerry Lampen/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Duterte amesema amefikia maamuzi ya nchi yake kujiondoa kwenye mkataba wa Roma uliounda Mahakama hiyo kwa kile alichokieleza ni kwa sababu ya kushambuliwa na Umoja wa Mataifa lakini pia ukiukwaji wa utaratibu na Mahakama hiyo.

Hatua hii imekuja baada ya Mahakama hiyo yenya makao yake mjini Hague nchini Uholanzi kuanza mchakato wa kuchunguza kampeni ya serikali yake kuhusu biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini humo.

“Naamua kutoa taarifa kuhusu Ufilipino kujiondoa kwenye mkataba wa Roma mara moja,” alisema rais Duterte kupitia kwa taarifa iliyotumwa kwa wanahabari.

Mahakama hiyo ilitangaza mwezi uliopita kuanzisha uchunguzi wa awali, kubaini iwapo uhalifu wa kivita na makosa mengine ya ukiukwaji wa haki za binadamu ulikuwa umetekelezwa wakati wa operesheni hiyo.

Polisi nchini Ufilipino wanasema watu 4,000 wameuawa katika operesheni hiyo lakini mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema idadi hiyo inaweza kuwa mara tatu au nne zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.