Pata taarifa kuu
AJALI-BANGLADESH-NEPAL

Ajali ya ndege nchini Nepal yasababisha vifo vya abiria 49

Watu 49 wameuawa na wengine  kujeruhiwa baada ya ndege ya abiria ya  Bangladesh iliyokuwa na abiria 71 kuanguka wakati ikitua katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kathmandu nchini Nepal.

Ndege ya abiria iliyoanguka ikiteketea moto  katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kathmandu nchini Nepal Machi 12 2018
Ndege ya abiria iliyoanguka ikiteketea moto katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kathmandu nchini Nepal Machi 12 2018 Twitter
Matangazo ya kibiashara

Maafisa nchini Nepal wanasema abiria 17 waliokolewa baada ya ajali hiyo huku wengine wengine wakipoteza maisha.

“Watu 31 waliuawa papo hapo na wengine tisa wakapoteza maisha wakiwa hospitalini jijini Kathmandu,” amesema msemaji wa Polisi Manoj Neupane.

Ndege hiyo ilikuwa imetokea jijini Dhaka, ikielekea jijini Kathmandu.

Moto mkubwa na moshi mzito ulishuhudiwa pindi tu ndege hiyo ilipoanguka na maafisa wamekuwa na kazi ngumu ya kujairbu kuuzima ili kuona iwapo itawaokoa abiria.

Uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali ya ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Marekani, US-Bangla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.