Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-MAREKANI

Korea Kusini: Hatujapata taarifa kutoka Korea Kaskazini kuhusu mazungumzo

Korea Kusini inasema haijapata jibu lolote kutoka Korea Kaskazini, baada ya tangazo la wiki iliyopita kuwa Kim Jong-un atakutana na rais wa Marekani Donald Trump mwezi Mei.

Kiongozi wa Korea Kaskazini  Kim Jong
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili lilitolewa na afisa wa juu wa serikali ya Korea Kusini Chung Eui-yong, baada ya kukutana na rais Trump jijini Washington DC, na kuarifu kuwa rais Trump alikuwa amekubali ombi la kukutana na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini.

Wizara inayoshughulikia muungano wa eneo la Korea, imesema Seoul haijapata taarifa yoyote kutoka Pyongyang.

Trump amenukuliwa akisema alikubali kukutana na Kim Jong-un baada ya Pyongyang kusema iko tayari kuachana na mradi wake wa kuzalisha silaha za nyuklia.

Hadi sasa, haijafahamika ni wapi mkutano huo utafanyika, wakati huu Korea Kusini ikiendelea na mipango ya kufanikisha kukutana kwa viongozi hao wawili.

Korea Kusini imemtuma afisa wake nchini China na Japan kuwaeleza viongozi wa nchi hizo kuhusu mipango ya mkutano huo.

Wachambuzi wa siasa za Kimatafa wanaonya kuwa licha ya tangazo hili, chochote kinawe kutokea kwa sababu huenda mkutano huo ukafanyika au usifanyike.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.