rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Korea Kaskazini Marekani Mike Pence

Imechapishwa • Imehaririwa

Korea Kaskazini yafuta mkutano na Mike Pence

media
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence. REUTERS/Ammar Awad

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence alikuwa tayari kukutana na ujumbe wa maafisa waandamizi wa Korea Kaskazini kando ya mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi lakini hii "mkutano huo" ulifutwa ¬ędakika za mwisho" na Pyongyang.


Mkutano huo ulifutwa na serikali ya Korea Kaskazini baada ya kauli nzito ya Bw Pence, serikali ya Marekan imetangaza.

Maafisa wa Marekani wanasema wajumbe wa Korea Kaskazini walijiondoa ghafla kutoka kwa mkutano wa faraghani uliokuwa umepangwa kufanyika mjini Seoul, Korea Kusini saa mbili kabla ya mkutano huo kufanyika.

Wakati wa ziara ya Mike Pence katika mji wa Pyeongchang, nchini Korea Kusini, kwenye ufunguzi wa mashindano ya Olimpiki, "kulikuepo na uwezekano wa mkutano mfupi na viongozi wa ujumbe wa Korea Kaskazini," amesema Msemaji wa wizara ya mashauriano ya kigeni ya Marekani Heather Nauert.

Makamu wa Rais alikuwa tayari kuchukua fursa hii ili kuonyesha haja ya Korea ya Kaskazini kuachana na mipango yake isio halali nyuklia na majaribio ya makombora ya masafa marefu, "amesema katika taarifa yake.

"Dakika za mwisho, Maafisa wa DPRK (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea) waliamua kutoendelea na mkutano huo. Tunasikitishwa sana na kukosa kwao kutumia fursa hii," ameongeza Healther Nauert.