Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-UGAIDI

Afghanistan yaomboleza vifo vya zaidi ya watu 100 jijini Kabul

Watu zaidi ya 100 wamethibitishwa kupoteza maisha jijini Kabul nchini Afganistan baada ya mlipuko wa bomu ndani ya gari la kubeba wagonjwa siku ya Jumamosi.

Gari la wagonjwa lilotumiwa kutekeleza shambulizi la bomu jijini Kabul nchini Afghanistan
Gari la wagonjwa lilotumiwa kutekeleza shambulizi la bomu jijini Kabul nchini Afghanistan REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Afganistan imetangaza siku tatu za maombolezo na kulaani shambulizi hilo la kigaidi.

Kundi la Taliban limekiri kutekeleza shambulizi hilo baya jijini Kabul katika siku za hivi karibuni.

Ripoti zinasema kuwa, walipuaji waliendesha gari hilo la wagojwa kulipokuwa mkusanyiko wa watu na kujilipua.

Waziri wa Mambo ya ndani Wais Barmak amesema watu wengi walipoteza maisha wakati wakipata matibabu hospitalini na watu wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa, hasa wanaume.

Shambulizi hili limezua hali ya wasiwasi jijini Kabul, na kusababisha watu wengi kuamua kusalia majumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.