Pata taarifa kuu
UNSC-IRAN-NYUKLIA-USALAMA

Umoja wa Mataifa kukagua mabaki ya silaha zilizotengenezwa Iran

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa watakwenda jijini Washingtin DC nchini Marekani siku ya Jumatatu, kukagua mabaki ya silaha za nyuklia, ambazo zinaaminiwa kutolewa na Iran kuwasaidia waasi wa Kihuthi nchini Yemen.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanatarakia kukutana na rais Donald Trump kujadili hatua ya kuichukulia Iran.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanatarakia kukutana na rais Donald Trump kujadili hatua ya kuichukulia Iran. REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Mbali na ukaguzi huo, wajumbe hao watakutana na rais Donald Trump kujadili hatua ya kuichukulia Iran.

Marekani kupitia kwa Balozi wake katika Baraza hilo Nikki Haley amesema ushahidi upo kuthibitisha kuwa wahusika ni Iran licha ya kukanusha madai hayo.

Hivi karibuni Rais wa Marekani Donald Trump alisema nchi yake inasitisha vikwazo dhidi ya Iran kwa mara ya mwisho, ili kutoa nafasi kwa bara la Ulaya na Marekani kuthathmini upya mkataba kuhusu mradi wa nyuklia wa Iran.

Rais Trump amekuwa akishtumu mkataba ulioafikiwa kati ya Mataifa ya Magharibi na Iran, kusitisha mradi huo hadi mwaka 2025, kuwa mbovu.

Badala yake, Trump anataka mkataba huo kuangaliwa upya na kurekebishwa kwa lengo la kuizua kaboa Iran kuendelea na mradi huo.

Msimamo wa Marekani unaungwa mkono na Israel ambayo imeendelea kuamini kuwa mradi huo wa nyuklia wa Iran, unalenga kuishambulia kutumia silaha za maangamizi.

Wiki mbili zilizopita, Iran kupitia Waziri wake wa Mambo ya nje Mohammad Javad Zarif alisema Marekani kuendelea na vitisho hivyo ni ishara ya kutotaka kutekelezwa kwa mkataba huo.

Mataifa ya Ulaya yakiongozwa na Ufaransa, Uingereza na Ujerumani yalimtaka rais Trump kukubali kutekelezwa kwa mkataba huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.