rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Iran Hassan Rouhani

Imechapishwa • Imehaririwa

Zaidi ya watu 440 waachiwa huru baada ya maandamano Iran

media
Watu wakiandamana karibu na chuo Kikuu cha Tehran Desemba 30, 2017. STR / AFP

Mamlaka nchini Iran imewaachia huru watu zaidi ya 440 waliokamatwa katika mji wa Tehran wakati wa maandamano dhidi ya serikali mwishoni mwa mwezi Desemba, mwendesha mashitaka wa Tehran amesema leo Jumatatu.

 


"Watu zaidi ya 440 waliokamatwa wakati wa maandamano dhidi ya serikali katika mji wa Tehran wameachiwa huru," Jafari Dolatabadi alinukuliwa na shirika la habari la Mehr akisema.

Watu wapatao 25 walikufa wakati wa maandamano ambayo hapo awali yalikuwa na lengo la kupinga mfumuko wa bei na hali ya maisha kuwa mbaya laikini maandamano hayo yaligeuzwa na yakaonekana ni yenye lengo la kupinga viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa maafisa wa mahakama, maelfu ya watu walikamatwa nchini Iran, idadi ambayo imekosolewa kwa mujibu wa mbunge Mahmoud Sadeghi ambaye amesema angalau watu 3,700 walikamatwa.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema wafungwa kadhaa walikufa wakati walipokua wakizuiliwa katika magereza.