rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Pakistani India Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Maandamano yaendelea kwenye mpaka wa Pakistan na India

media
Maandamano ya watu wenye hasira dhidi ya mauaji ya msichana mmoja raia wa Pakistan. REUTERS/Saeed Ali Achakzai

Mamia ya waandamanaji wenye hasira wameandamana kwenye mji wa Pakistani ulio karibu na mpaka na nchi ya India, wakirusha mawe kulenga ofisi za Serikali kuonesha hasira dhidi ya mauaji ya msichana mmoja raia wa nchi hiyo.


Waandamanaji walirusha mawe kulenga hospitali na kushambulia makazi ya mwanasiasa mmoja kwenye mji wa Kasur jimboni Punjab wakiwalaumu polisi kwa kushindwa kushughulikia suala la kuuawa kwa msichana huyo.

Maandamano yalianza juma hili wakati wananchi walipouokota mwili wa msichana huyo katika jalala moja katika kile ambacho kinaonekana alitupwa hapo baada ya kubakwa na kundi la watu.

Polisi wanasema kuwa msichana huyo alikuwa na umri wa miaka 8 na vipimo vimeonesha alibakwa kabla ya kuuawa.