Pata taarifa kuu
EU-IRAN-USALAMA

EU yaunga mkono mkataba wa nyuklia kati yao na Iran

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Federica Mogherini eo Alhamisi amesema kuwa makubaliano ya mkataba wa nyuklia uliotiwa saini kati ya nchi zao na Iran unafanya kazi, wakati huu Marekani ikitishia kuiwekea vikwazo zaidi nchi hiyo.

Mogherini anasema  mkataba wa nyuklia kati ya nchi za Ulaya na Iran "unafanya kazi,kwa salama wa dunia na unazuia utengenezaji wa silaha za nyuklia katika kanda Aia ya magharibi".
Mogherini anasema mkataba wa nyuklia kati ya nchi za Ulaya na Iran "unafanya kazi,kwa salama wa dunia na unazuia utengenezaji wa silaha za nyuklia katika kanda Aia ya magharibi". REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Mogherini amesema haya baada ya kukutana na ujumbe wa Iran ulioongozwa na waziri wa mambo ya kigeni Mohammad Javad Zarif, ambapo amesema vikwazo vya Marekani havitakwamisha juhudi zao za utekelezaji makubaliano waliyotiliana saini na Iran kuhusu mpango wake wa Nyuklia.

Hivi karibuni rais Donald Trump amesema nchi yake itaiwekea vikwazo zaidi Iran na kutangaza nchi yake kujitoa kwenye makubaliano yaliyofikiwa na mtangulizi wake Barack Obama.

Trump aliskosoa vikali mkataba huo akisema kuwa ni upuuzi mtupu.

Hata hivyo Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema mkataba huo uliokosolewa na rais wa Marekani Donald Trump unatumika sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.