rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Korea Kusini Korea Kaskazini Moon Jae-in Kim Jong Un

Imechapishwa • Imehaririwa

Rais wa Korea Kusini akubali kukutana na mwenzake wa Kaskazini

media
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in anasema yuko tayari kukutana kwa mazungumzo na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, January 10, 2018. REUTERS/Kim Hong-Ji

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In amesema yuko tayari kuzungumza na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un katika siku zijazo.


Hatua hii imekuja, baada ya nchi hizi mbili jirani kutia saini makubaliano baada ya siku mbili za mazungumzo kuhusu, Korea Kaskazini kutuma wanariadha wake katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi mwezi ujao nchini Korea Kusini.

Rais Moon amesema kuwa, anaamini kuwa baada ya mwafaka huu, ni mwanzo mzuri wa mambo mazuri kati ya mataifa hayo mawili.

Aidha, ameongeza kuwam ili kupata amani ya kudumu katika eneo la Korea, ni lazima Korea Kaskazini iachane kabisa na mradi wake wa kutengeza silaha za nyuklia.

Kiongozi huyo amesisitiza kuwa, yuko tayari kukutana na Kim Jong iwapo mazingira yataruhusu katika siku zijazo, kujadili suala hili na kupata mwafaka.

Marekani nayo imekuwa ikisema kuwa iko tayari kuzungumza na Korea Kaskazini, iwapo itasitisha mradi wake wa nyuklia.

Rais Donald Trump ambaye serikali yake imekuwa ikiweka vikwazo dhidi ya Pyongyang, amesema vikwazo hivyo, vimesaidia kufanyika kwa mazungumzo hayo.