rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Korea Kusini Korea Kaskazini Moon Jae-in Kim Jong Un

Imechapishwa • Imehaririwa

Moon azungumzia njia ya kupata amani katika ukanda wa Korea

media
Kiongozi wa Korea Kusini Moon Jae-In ©REUTERS/Nicolas Asfouri/Pool

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In amesema, eneo la Korea kutokuwa na mradi wa kutengeneza silaha za nyuklia ndio njia pekee ya kupata amani.


Aidha, amesema atakuwa tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un iwapo mazingira yataruhusu ili kuendelea kujadili suala hili.

Kauli ya rais Moon imekuja baada ya mataiafa hayo mawili jirani kuanza mazungumzo siku ya Jumanne kwa mara ya kwanza baada ya mwaka 2015.

Lengo la mazungumzo hayo, ni kwa Korea Kusini kuiruhusu Korea Kaskazini kutuma kikosi cha wanamichezo wake kushiriki mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi mwezi ujao.