Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI-USHIRIKIANO

Seoul yapendekeza mazungumzo na Pyongyang

Korea Kusini imependekeza mazungumzo ya kiwango cha juu na Korea Kaskazini tarehe 9 Januari mwaka huu, baada ya kuingizi wa korea Kaskazini Kim Jong-Un kutoa wito kwa jirani yake kuimarisha uhusiano mzuri wa nchi hizo mbili.

Kiongozi wa Korea Kusini, Moon Jae-in.
Kiongozi wa Korea Kusini, Moon Jae-in. The Presidential Blue House/Yonhap via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Rais Kim Jong-un pia alitoa wito wa kujadili ushiriki wa Korea Kaskazini katika Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini .

Kiongozi wa Korea Kaskazini alitumia fursa hiyo alipokua akihitubia wananchi wake akiwatakiwa heri ya Mwaka Mpya. Wakati huo rais wa Korea Kaskazini alisema kuwa kitufe cha kurusha makombora ya nyuklia kipo siku zote kwenye meza yake, onyo ambalo amelitoa kwa Marekani.

Waziri wa Muungano wa Korea Kusini Cho Myoung-Gyon ameelezea kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa nchi yake " ina nia nzuri ya kufanya na mazungumzo na Korea Kaskazini wakati wowote, mahali popote na katika hali yoyote".

"Tunatarajia kwamba Korea Kusini na Korea Kaskazini zitaweza kukaa pamoja ili kujadili ushiriki wa Korea Kaskazini katika Michezo ya Olimpiki ya Pyeongchang na hata kujadili masuala mengine ya maslahi ya pamoja kwa kuboresha mahusiano ya Korea zote mbili," Waziri Myoung-Gyon ameongeza.

Tangu mwisho wa Vita vya Korea (1950-53),nchi hizi mbili hasimu zinatenganishwa na eneo la mpakani (DMZ), mojawapo ya maeneo ya mpakani yenye askari wengi duniani. Mazungumzo ya hivi karibuni ya nchi hizi mbili yalifanyiika mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.