Pata taarifa kuu
IRAN-SIASA-UCHUMI

Maelfu waandamana dhidi ya serikali ya Iran

Waandamanaji nchini Iran wamefurika katika miji mbambali kulalamikia kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali nchini humo.

Kiongozi wa Iran Hassan Rouhani
Kiongozi wa Iran Hassan Rouhani ACI
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya waandamanaji wameonekana katika miji ya Kusini na Kaskazini, wakiimba nyimbo na kubeba mabango wakionesha hasira zao dhidi ya sera za serikali ya Tehran wanazosema, zimesababisha gharama ya maisha kupanda.

Aidha, waandamanaji wanamlaumu rais Hassan Rouhani kwa kuleta sera ambazo zimeyumbisha uchumi wa nchi hiyo.

Ripoti zinasema kuwa waandamanaji kadhaa wamekamatwa katika makabiliano na polisi wa kupambana na ghasia.

Marekani imeunga mkono maandamano hayo, na kuyataka mataiffa ya dunia kusimama na watu wa Iran wanaopigania haki zao na kupambana na ufisadi.

“Serikali ya Iran ina jukumu la kuheshimu haki za watu, haki ya kujieleza. Dunia inatazama,” amesema msemaji wa Ikulu ya Marekani Sarah Huckabee Sanders.

Haya ndio maandamano makubwa dhidi ya serikali tangu mwaka 2009 nchini humo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.