Pata taarifa kuu
BURMA-MSF-HAKI

MSF: Watu 6,700 kutoka jamii ya Rohingya waliuawa Burma

Watu wasiopungua 6,700 kutoka jamii ya Rohingya, ikiwa ni pamoja na watoto 730 walio na umri ulio chini ya miaka mitano, waliuawa mwezi wa kwanza wa operesheni ya kijeshi, magharibi mwa Burma kati ya Agosti 25 na Septemba 25, kwa mujibu washirika la Madaktari wasio na Mipaka (MSF).

wakimbizi wa Rohingya wakiwasili katika kambi ya Teknaf, Bangladesh, Oktoba 25, 2017.
wakimbizi wa Rohingya wakiwasili katika kambi ya Teknaf, Bangladesh, Oktoba 25, 2017. REUTERS/Hannah McKay
Matangazo ya kibiashara

Idadi hiyo huenda ikawa juu ya hiyo tuliotoa," amesema Dk. Wong wa MSF, ambaye aliwahoji wakimbizi zaidi ya 11,000 nchini Bangladesh.

Zaidi ya Waislamu 640,000 wa jamii ya Rohingya wamekimbilia Bangladesh tangu mwishoni mwa mwezi Agosti kufuatia kile Umoja wa Mataifa umekitaja kuwa ni "kuangamiza ukabila".

Hadi sasa, jeshi la Burma limebaini kwamba limefaulu kuwaua watu 400 kwa upande wa "magaidi" wa Rohingya ambao walianzisha vita mwishoni mwa mwezi Agosti.

Takwimu za MSF zinaonyesha tu mwezi wa kwanza wa vurugu, lakini watu kutoka jamii hiyo wanaendelea kutoroka makazi yao hadi leo na watu wanaokimbia "wanasema wamenyanyaswa katika wiki za hivi karibuni."

Kwa mujibu wa MSF, "vitendo vivyo viovu vinavyofanyiwa jamii ya Rohingya vinatisha".

"Tumewasikia watu wanasema kwamba familia zote ziliuawa baada ya vikosi vya Burma kuwafunganiana ndani ya nyumba zao kabla ya kuzichoma moto," amesema Dk. Wong.

Uchunguzi unaonyesha kuwa 69% waliuawa kwa risasi, 9% waliuawa kwa kuchomwa moto na 5% waliuawa kwa kupigwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.