Pata taarifa kuu
KOREA-KUSINI-CHINA-USALAMA

Beijing na Seoul: Hakuna vita vitakavyotokea katika rasi ya Korea

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae-in wametangaza leo Alhamisi kwamba hawatokuba vita kutokea katika rasi ya Korea, shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap limearifu.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In (kushoto) na rais wa China Xi Jinping (kulia) katika Ikulu ya Great Hall of the People Beijing tarehe 14 Desemba 2017.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In (kushoto) na rais wa China Xi Jinping (kulia) katika Ikulu ya Great Hall of the People Beijing tarehe 14 Desemba 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili zitashirikiana katika utekelezwaji wa vikwazo na katika kuishinikiza Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia na majaribio yake ya makombora ya masafa marefu, shirika la habari la Yonhap limeongeza.

Lengo la kuachana na utengenezaji wa silaha za nyuklia linapaswa kuzingatiwa katika rasi ya Korea, hivyo vita na machafuko kutopewa nafasi katika kanda hiyo, pia amesema Xi Jinping, ambaye alikutana na rais wa Korea Kusini mjini Beijing.

"Tatizo larasi ya Korea linapaswa kutatuliwa kupitia mazungumzo na mashauriano," Xi ameongeza.

Kwa upande wake Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema anatarajia kushirikiana na Marekani ili kupata suluhisho la mgogoro wa Korea.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In (katikati) na rais wa China Xi Jinping (kushoto) wakikagua kikosi cha ulinzi wa taifa wakati wa sherehe ikulu ya Great Hall of the People, Beijing Desemba 14, 2017.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In (katikati) na rais wa China Xi Jinping (kushoto) wakikagua kikosi cha ulinzi wa taifa wakati wa sherehe ikulu ya Great Hall of the People, Beijing Desemba 14, 2017. AFP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.