Pata taarifa kuu
CHINA-SIASA-USALAMA

Xi Jinping atoa wito wakupambana kwa kile kinachoweza kuhatairisha utawala wake

Kiongozi wa China Xi Jinping amewataka wafuasi wake wa chama cha kikomunisti cha PCC kupambana na jambo lolote linaloweza kutishia mamlaka ya chama tawala.

Rais wa China Xi Jinping akifungua kongamano la 19 la Chama Cha Kikomunisti nchini China, Oktoba 18, 2017 Beijing.
Rais wa China Xi Jinping akifungua kongamano la 19 la Chama Cha Kikomunisti nchini China, Oktoba 18, 2017 Beijing. REUTERS/Jason Lee
Matangazo ya kibiashara

Xi Jinping ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 19 wa chama chake utakaompa fursa ya kuendelea kuongoza taifa la China lenye watu wengi zaidi duniani.

Bw. Jinping ameahidi "enzi mpya" za kisoshalisti nchini kwake, na kufuta matumaini ya kuachia ngazi. Katika hotuba yake ilidumu zaidi ya saa tatu, amesem ayuko tayari kuongoza hadi mwaka 2050.

"Sisi sote ni lazima tushirikiane kwa kulinda mamlaka ya chama tawala na mfumo wa kisoshalisti nchini China na kupinga kauli yoyote na hatua inavyoweza kuhatarisha utawala wetu," amebaini Rais wa China, mbele ya wajumbe 2,300 walikusanyika kwa kongamano kuu la chama cha PCC linalofanyika kila baada ya miaka mitano.

Karibu wajumbe wote wa chama hiki wakivalia suti nyeusi na tai nyekundu, walisikiliza kwa makini hotuba ya kiongozi wao kutoka jengo la bunge la Beijing, baada ya kumpongeza alipoingia katika ukumbi wa jengo hilo kama kiongozi pekee anayefaa kuongoza China. Xi Jinping aliongozana katika sherehe za ufunguzi wa kongamano hilo na watangulizi wake wawili, marais wa zamani Jiang Zemin na Hu Jintao.

Chama cha PCC ndio chama kikubwa duniani chenye wafuasi milioni 89.

Xi alisema nchi yake "itafungua njia kwa makampuni ya kigeni" na kuahidi "kushughulikia sawa" kwa makampuni ya kigeni.

Wakati huu mechi za soka zimepigwa marufuku, klabu za usiku zimefungwa. Wakati huu mji mkuu wa China uko chini ya ulinzi mkali, na kongamano hili litaumu wiki moja

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.