Pata taarifa kuu
JAPAN-INDIA-USHIRIKIANO

Japan yazindua mradi wa ujenzi wa treni ya mwendo kasi India

Waziri Mkuu wa Japan anazuru Alhamisi hii India, na hasa katika jimbo la Gujarat, ambapo amezindua mradi muhimu, mradi ambao umeanzisha kujengwa kwa treni ya kwanza ya mwendo kasi, kwa kutumia teknolojia ya Japan.

WAziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe (kushoto) na mwenziie wa India Narendra Modi, wakati wa uzinduzi wa mrandi wa ujenzi wa  treni ya kwanza ya mwendo kasi Septemba 14, 2017 Ahmedabad.
WAziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe (kushoto) na mwenziie wa India Narendra Modi, wakati wa uzinduzi wa mrandi wa ujenzi wa treni ya kwanza ya mwendo kasi Septemba 14, 2017 Ahmedabad. REUTERS/Amit Dave
Matangazo ya kibiashara

Bw. Abe anafanya ziara ya siku mbili nchini India ambayo ni mshirika mkuu wa Japan.

Treni hii ya teknolojia ya Japan itaunganisha safari ya kwenda Ahmedabad, na Goujarat, na ile ya Bombay kwa muda wa saa 3 ikilinganishwa na saa 8 ile ya sasa.

Changamoto bado zipo. Upatikanaji wa ardhi muhimu itakuwa ngumu katika nchi hii kubwa ya kilimo ambapo mashamba yamegawanywa katika viwanja vidogo.

Mradi huo utaanza kutoa huduma katika kipindi cha miaka mitano, safari ya kilomita 500 inatarajiwa kupunguzwa hadi masaa matatu kutoka masaa manane ya kawaida.

Treni hiyo ya viti 750 inatarajiwa kuanza kuhudumua kuanzia Agosti mwaka 2022.

Mifumo ya usafiri wa treni nchini India husafirisha zaidi ya watu milioni 22 kwa siku na baadhi ya treni zimepitwa na wakati hali ambayo huchangia ajali za mara kwa mara.

Nauli ya kwa kutumia treni hii pia itakua kubwa zaidi kuliko ile ya sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.