Pata taarifa kuu
MYANMAR-MAUAJI-USALAMA

Aung San Suu Kyi kuzungumzia upatano wa kitaifa na amani

Kiongozi wa Myanmar Aung San Suu Kyi wiki ijayo atalihutubia taifa kuelezea mgogoro kwenye jimbo la Rakhine, hotuba yake ya kwanza tangu kuuawa kwa maelfu ya raia wa Rohingya wanaokimbilia nchini Bangladesh.

Aung San Suu Kyi hatahudhuria mkutano Mkuu unaowakutanisha viongozi wa dunia katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wiki ijayo.
Aung San Suu Kyi hatahudhuria mkutano Mkuu unaowakutanisha viongozi wa dunia katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wiki ijayo. REUTERS/Soe Zeya Tun
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa Serikali Zaw Htay, amesema kuwa Suu Kyi atahutubia taifa kuzungumzia upatano wa kitaifa na amani katika hotuba itakayorushwa na televisheni ya taifa.

Aung San Suu Kyi ambaye kwa majuma kadhaa amekuwa kwenye shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa akikosolewa kwa kushindwa kukemea mauaji dhidi ya raia wa Rohingya, atakosa pia kuhudhuria mkutano wa baraza la umoja wa Mataifa unaoanza wiki ijayo.

Machafuko kwenye jimbo hilo yamesababisha janga la kibinadamu na wakimbizi kwenye maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Bangladesh hali iliyoamsha hasira toka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu yanaoukashifu utawala wa Myanmar kwa kuzembea.

Mpaka sasa jumla ya raia wa Rohingya laki 3 na elfu 79 wamekimbilia nchini Bangladesh katika kipindi cha wiki tatu zilizopita.

Hayo yakijiri Aung San Suu Kyi hatahudhuria mkutano Mkuu unaowakutanisha viongozi wa dunia katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wiki ijayo.

Hili limebainika hasa wakati huu, anapoendelea kushtumiwa kwa kutochukua hatua za kutosha kuzuia kushambuliwa na kuuawa kwa Waislamu wa jamii wa Rohingya nchini mwake.

Watu wapatao 370,000 wa jamii ya hiyo ya Rohingya wamekimbilia nchini Bangladesha kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.