Pata taarifa kuu
MYANMAR-MAUAJI-USALAMA

Nchi za Kiislam zashtumu dhulma dhidi ya Warohingya

Muungano wa nchi za Kiislamu duniani, unalaani mauaji na mashambulizi dhidi ya Waislamu kutoka jamii ya Rohingya nchini Mynamar.

Waakimbizi wa Rohingya wakivuka mpaka kati ya Myanmar na Bangladesh, katika eneo la Bazar, nchini Bangladesh, Septemba 9, 2017.
Waakimbizi wa Rohingya wakivuka mpaka kati ya Myanmar na Bangladesh, katika eneo la Bazar, nchini Bangladesh, Septemba 9, 2017. REUTERS/Danish Siddiqui
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa unasema kuwa watu 300,000 wameyakimbia makwao na kuingia nchini Bangladesh kwa kuhofia mashambulizi katika jimbo la Rakhine.

Serikali ya Mynmar imelaumiwa kwa kushindwa kuwazuia vikosi vyake vya usalama na makundi mengine kuwavamia Waislamu hao.

Tangu Agosti 25, jeshi la Burma lilianzisha ukandamizaji dhidi ya jamii ya watu wachache wa Rohingya,hali ambayo ilisababisha watu 300,000 kukimbilia nchini Bangladesh. Chuki la jeshi kwa jamii hii ya watu wachache wa Kiislamu ni ya toka zamani katika nchi hii ya yenye waumini wengi wa dini ya Kibudha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.