Pata taarifa kuu
URUSI-KOREA KASKAZINI-MAREANI-USALAMA

Urusi yapuuzia vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini

Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov ameionya Marekani kuyapa kipaumbele mazungumzo kuliko kuiweka vikwazo zaidi Korea Kaskazini.

Waziri wa mashauriano ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov aionya Marekani vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini haivitabadili chochote..
Waziri wa mashauriano ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov aionya Marekani vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini haivitabadili chochote.. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amemueleza Waziri wa Ulinzi wa Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini ni kama kumwagia maji kwenye mgongo wa bata.

Hata hivyo Bw.Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana.

Waziri wa Ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini.

Kulingana na taarifa ya wizara ya kigeni ya Urusi, Sergei Lavrov na Rex Tillerson walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Korea Kaskazini.

Siku moja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani jaribio la Korea Kaskazini Siku ya Jumatano, rais wa Marekani Donald Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo na Korea Kaskazini sio suluhisho.

Mapema wiki hii Korea Kaskazini ilirusha kombora lake la masafa marefu lililopitia juu ya anga ya Japan, kitendo ambacho Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alisema ni uchokozi wa Korea Kaskazini unaoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.