Pata taarifa kuu
INDIA-USALAMA

Mhubiri mkuu akutwa na hatia ya ubakaji India

Eneo la kaskazini mwa India linakabiliwa na machafuko, siku mbili baada ya mhubiri mkuu Gurmeet Ram Rahim Singh kukutwa na hatia ya ubakaji.

Barabara zote zinazoelekea jela la Sunariya katika mji wa Rohtak ambako anazuiliwa mhubiri mkuu wa dini Ram Rahim Singh zimemefungwa.
Barabara zote zinazoelekea jela la Sunariya katika mji wa Rohtak ambako anazuiliwa mhubiri mkuu wa dini Ram Rahim Singh zimemefungwa. REUTERS/Adnan Abidi
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama katika jimboni Haryana na Punjab, kaskazini mwa India wamekuwa katika tahadhari ya hali ya juu kabla ya hukumu tata dhidi ya mhubiri mkuu huyo Jumatatu hii Agosti 28 mchana.

Maelfu ya askari wametumwa katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na jiji ambalo ni makao makuu ya dini anayoongoza Gurmeet Ram Rahim Singh. Wafuasi wa mhubiri huu mkuu, waliliokuja kumuunga mkono walisababisha vurugu katika mitaa ya miji kadhaa siku ya Ijumaa, baada ya kiongozi wao kukutwa na hatia ya ubakaji.

Vurugu hizi zilisababisha vifo vya watu 38 kulingana na ripoti ya hivi karibuni. Hatua kali zimewekwa ili kuzuia kuzuka upya kwa machafuko leo Jumatatu Agosti 28.

Kufuati hali hiyo Shule, vyuo na ofisi za serikali za Haryana zimeamriwa kufungwa katika mji wa Rohtak Jumatatu hii, na mtandao wa simu za mkononi utafungwa hadi siku ya Jumanne katika jimbo la kaskazini mwa India, kitovu cha uhasama wa siku ya Ijumaa.

Askari wengi wametumwa katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na Sirsa, ambapo ni makao makuu ya dini ya Dera Sacha Sauda, inayoongozwa na Ram Rahim Singh.

Katika siku mbili za zilizopita, wafuasi wake, wakiongozwa na jeshi, walilazimika kuondoka katika eneo la heka 400 la dini hiyo yenye waumini 10,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.