rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Ukraine

Imechapishwa • Imehaririwa

Pentagon kusaidia jeshi la Ukraine

media
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko akipeana mkono na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim Mattis Kiev tarehe 24 Agosti 2017. AFP

Mkuu wa Pentagon Jim Mattis amethibitisha Alhamisi hii mjini Kiev kwamba Marekani iko tayari kusaidia jeshi la Ukraine linalopambana kwa zaidi ya miaka mitatu dhidi ya waasi wanaounga mkono Urusi.


Hata hivyo Jim Mattis hajazungumzia iwapo Marekani iko tayari kusaidia jeshi la Ukraine vifaa vya kijeshi vinavyoweza.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani ametoa onyo kali dhidi ya Urusi, ambayo inashtumiwa kutaka "kukata upya mipaka ya kimataifa kwa nguvu", akionya kuwa vikwazo vinavyoilenga vitachukuliwa hadi pale Moscow itatekeleza mkataba wa amani wa Minsk kwa Mashariki mwa Ukraine.

Vita bado vinaendelea kati ya vikosi vya Ukraine na wapiganaji wanaoungwa mkono na Urusi. Vita hivi vimesababisha vifo vya watu kadhaa na maelfu ya watu kuyahama makazi yao.