Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani na Korea Kusini kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi

Marekani na Korea Kusini wanaanza mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyopangwa kufanyika leo Jumatatu Agosti 31, wakati ambapo mvutano na Korea Kaskazini ukiendelea.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in akimsabahi Joseph Dunford, Mkuu wa Majeshi ya Marekani, tarehe 14 Agosti 2017 Seoul.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in akimsabahi Joseph Dunford, Mkuu wa Majeshi ya Marekani, tarehe 14 Agosti 2017 Seoul. Bae Jae-man/Yonhap via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hilo linaashiria uwezekano wa vita na Pyongyang, ambayo inayachukulia mazoezi hayo ya kila mwaka kama uchokozi na uvamizi. Serikali ya Kim Jong-un imetishia kujibu vikali.

Korea Kaskazini tayari imelaani mazoezi hayo ikisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kumwaga mafuta kwenye moto.

Serikali ya Pyongyang imeonya mapema kwamba mazoezi hayo ya pamoja ya kijeshi yanaazimia kuongeza mvutano katika ukanda huo.

Maelfu ya askari wanashiriki katika zoezi hili linaloitwa "Ulchi Freedom Guardian" (UFG). Mazoezi haya yanafanyika nchini Korea ya Kusini na yatadumu wiki mbili.

Korea Kusini hutuma wanajeshi 50,000 huku Marekani nayo ikituma kati ya wanajeshi 25,000 na 30,000.

Mazoezi hayo hujumuisha ya ardhini , baharini na angani. Mazoezi hayo ambayo hufanyika Korea Kusini pia hujumuisha mafunzo jinsi ya kukabiliana na ugaidi na mashambulizi ya kemikali.

Korea Kaskazini tayari imelaani mazoezi hayo ikisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kumwaga mafuta kwenye moto.

Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilionekana kulegeza kamba baada ya kutisha kuwa itarusha makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, lakini tena ikasema kuwa itafuatilia mienendo ya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.