Pata taarifa kuu
CHINA-TABIA NCHI

Tetemeko kubwa kusini magharibi mwa China laua watu zaidi ya 13 China

Watu zaidi ya 13 wamepoteza maisha kufuatia tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.0 katika vipimo vya richter lililokumba mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China.

Maafisa wa kikosi cha uokoaji wakiendesha shughuli ya uokoaji katika kijiji cha Gengdi, katika mkoa wa Sichuan, baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi Agosti 8, 2017.
Maafisa wa kikosi cha uokoaji wakiendesha shughuli ya uokoaji katika kijiji cha Gengdi, katika mkoa wa Sichuan, baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi Agosti 8, 2017. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mkoa wa Sichuan umeendelea kushuhudia visa hivi kwa miaka kadhaa sasa. Mwaka 2008 watu zaidi ya 70,000 waliuawa wakati tetemeko lilikumba eneo hilo.

Baadhi ya ripoti zinasema kuwa idadi hii ya waliopoteza maisha inaweza kuongezea.

Tume ya taifa inayohusika na majanga nchini China ikinukuu shirika la habari la AFP ilisema kuwa hadi watu 100 wanaripotiwa kupotza maisha na nyumba 130,000 kuharibiwa.

Baadhi ya vyombo vya habari vya China vimearifu kuwa watalii ni miongoni mwa watu waliouwawa na kujeruhiwa.

Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa eneo lililo maarufu kwa watalii, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.