Pata taarifa kuu
JAPAN-KOREA KASKAZINI-VIKWAZO

Japan kuiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini

Japan inatazamia kuiwekea vikwazovipya Korea Kaskazini katika kukabiliana na mpango wake wa silaha, amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Fumio Kishida, saa chache baada ya Baraza la Seneti la Marekani kupiga kura ya kuziwekea vikwazo dhidi Urusi, Iran, na Korea Kaskazini.

((Kutoka Kushoto kwenda kulia) Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Fumio Kishida, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini Yun Byung-se na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, Seoul Machi 21, 2015.
((Kutoka Kushoto kwenda kulia) Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Fumio Kishida, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini Yun Byung-se na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, Seoul Machi 21, 2015. REUTERS/Kim Hong-Ji
Matangazo ya kibiashara

"Kwa kuwa hatuwezi kutarajia mazungumzo ya uhakika, shinikizo kwao ni muhimu," amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan kwa vyombo vya habari.

Hakuna pendekezo halisi lililotolewa kwa kutatua suala la raia wa Japan waliotekwa nyara na maafisa wa usalama wa Korea Kaskazini kwa mika kadhaa iliyopita, ameongeza Waziri Kishida.

Japan itachukua hatua zakuzuia mali za makampuni matano, ikiwa ni pamoja na mawili kutoka China, na mali za watu tisa, alisema Kishida.

Katibu dola wa JapanYoshihide Suga alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba makampuni haya "yalisiriki katika shughuli zilizopigwa marufuku na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa."

Japan inaendelea kuwasiliana na washirika wake muhimu kama Marekani na Korea ya Kusini, alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan.

Baraza la Seneti la Marekani lilipiga kura siku ya Alhamisi ya kuziwekea vikwazo vipya nchi za Urusi, Korea Kaskazini na Iran, licha ya pingamizi za Rais Donald Trump, ambaye hivi karibuni atatoa uamuzi wake wa kuunga au kupinga kura hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.