Pata taarifa kuu
PANAMA-CHINA-TAIWANI-USHIRIKIANO

Panama yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan

Panama imechukua uamuzi wa kuvunja uhusiano wake na Taiwana na imeamua kuboresha uhusiano wake na China. Panama na Taiwan ni nchi mbili ambazo zilikua na uhusiano wa muda mrefu.

China inayotumia mfereji wa Panama kwa safari za meli, imeongeza kiwango cha uwekezaji wake chini Panama katika miaka ya hivi karibuni.
China inayotumia mfereji wa Panama kwa safari za meli, imeongeza kiwango cha uwekezaji wake chini Panama katika miaka ya hivi karibuni. Jean-Philippe Boulet
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Taiwan, imesema imekasirishwa na hatua hiyo ya Panama kuanzisha uhusiano na China, huku ikasema kuwa haitashindana na China katika kile ilichokitaja kuwa mchezo wa pesa katika diplomasia.

China inayotumia mfereji wa Panama kwa safari za meli, imeongeza kiwango cha uwekezaji wake katika taifa hilo la Amerika ya kati katika miaka ya hivi karibuni.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya China katika taarifa, ilisema kuwa serikali ya China inakaribisha hatua hiyo ya Panama.

Serikali ya Panama imesema inatambua kuwa Tawan ni sehemu ya China, lakini tayari ni nchi huru sasa

China imebaini kwamba Taiwan ni moja ya mikoa yake uliojitenga lakini inasema ni vizuri Taiwan kurudi kuunganishwa na China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.